.

.

27 Juni 2015

RAIA WAKIGENI WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI KAGERA.


Jeshi la Polisi mkoani Kagera limefanikiwa kuwakamata raia watano wa kigeni wanaodhaniwa kuwa wametokea nchi za Elitria na Ethiopia waliopitia nchini Uganda na kuingia mjini Bukoba bila kufuata taratibu zinazohusika kwa kusingizia wanakwenda kufungua hoteli ya kimataifa jijini Dar es Salaamu huku wakiwa na dola elfu mbili miatano mfukoni.
Akiongea mjini Bukoba kamishina msaidizi wa jeshi la Polisi mkoani Kagera Gilles Mloto amesema jeshi la polisi liliwatilia mashaka raia hao wa kigeni mara baada ya kuwakuta katika basi la Sumri lililokuwa likitokea mkoani Kagera likielekea jijini Dar es Salaam na baada ya kufika katika kizuizi wilayani Biharamulo basi hilo lilikaguliwa na kubainika limebeba raia wa kigeni watano ambao sasa wamefikishwa katika kituo cha polis mjini Bukoba kwaajili ya upelezi zaidi.
Kamishina msaidizi wa jeshi la Polisi mkoani Kagera Gilles Mloto amesema raia hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika ili taratibu za kisheria ziweze kufuatwa.
Katika tukio jingine jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki mbili aina Shotigani ambazo zilikuwa zikitumika kufanya uwindaji haramu katika pori la akiba la kimisi na kwamba majingili waliokamatwa na silaha hizo pia walikutwa na mnyama aina swala ambae walikuwa wamemuuwa katika pori hilo la kimisi lililopo wilayani Karagwe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni