.

.

20 Septemba 2015

HAYA NDIO MANENO ALIYOZUNGUMZA BEN CARSON AMBAYE ANAWANIA URAIS MAREKANI KUPITIA CHAMA CHA REPUBLICAN.



Mmoja wa wanasiasa wanaowania kuchaguliwa kugombea urais kwa niaba ya chama cha Republican,nchini Marekani amesema Uislamu hauambatani na katiba ya taifa hilo.
Ben Carson,ambaye ni, daktari wa neva aliyestaafu, amesema yeye katu hawezi kukubali Muislamu kuwa rais wa Marekani.
Akijibu maswali katika kipindi cha mahojiano cha runinga ya NBC ''Meet the Press,Carson anasema kuwa dini hiyo inakinzana na katiba ya Marekani.
Kura ya maoni inaonesha kuwa daktari huyo ambaye ni mkristo anashikilia nafasi ya pili kwa umaarufu nyuma ya bilionea mbishi Donald Trump.
Matamshi yake yanatokea siku chache, baada ya mgombea anayepigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republican, Donald Trump, kukataa kujitenga na mfuasi wake, ambaye alimshutumu Rais Obama kuwa Muislamu, na hata sio Mmarekani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni