Simba SC leo imeibuka kifua mbele baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao
3-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyopigwa katika Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao yote ya Wekundu wa Msimbazi
yamewekwa kimiani na mshambuliaji raia wa Uganda, Hamis Kiiza aliyepiga
'hat trick' na kuondoka na mpira wake baada ya mechi.
Bao pekee la Kagera Sugar limefungwa na Mbarak Yusuf.
Kwa matokeo ya leo, Simba wamefikisha jumla ya pointi 9 wakiwa wamecheza michezo mitatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni