.

.

07 Februari 2016

JE WAELEWA NINI JUU YA UGONJWA WA FIBROIDS?


Fibroids maana yake ni uvimbe wa msuli wa
kifuko cha uzazi. Uvimbe huu unaweza kuwa
na ukubwa tofauti kuanzia kama punje ya
harage mpaka ukubwa wa nazi. Wakati
mwingine unaweza kudhani ni ujauzito!
Sio kila mwenye fibroids anakuwa na matatizo
kiafya. Zinaweza kuwepo miaka mingi bila
matatizo yoyote. Hata hivyo inashauriwa kila
mwenye fibroids awe anapimwa na daktari
angalau mara moja kwa mwaka ili kuona jinsi
zinavyoendelea na kuhakikisha kuwa hazikui
kwa kasi au kuhatarisha kuwa kansa.
Kwa wale zinaowaletea matatizo, fibroids
husababisha kutokwa na damu nyingi za
hedhi, maumivu ya tumbo, mimba kuharibika
zikiwa changa, kuzaa watoto njiti na fibroid
kukandamiza viungo vingine kama kibofu cha
mkojo na kusababisha kukojoa mara kwa mara
au matatizo ya haja kubwa.
Njia ya kugundua uwepo wa fibroid ni kupimwa
na daktari na kufanyiwa ultrasound.
Matibabu yake yapo ya aina kuu tatu:
1. Kunywa dawa. Hata hivyo dawa zilizopo
sasa hazina matokeo mazuri kuondoa fibroids
ila husaidia kupunguza ukuaji wake.
2. Kuiondoa fibroid kwa operation. Ziko aina
nyingi za operation kupitia kwenye tumbo au
kupitia ndani ya kifuko cha uzazi. Aina ya
operation hutegemea mahali ilipo fibroid.
3. Kuondoa kifuko cha uzazi. Njia hii huwafaa
wale ambao hawana mpango wa kupata
mtoto.
Kuna nadharia mbalimbali juu ya vitu
vinavyosababisha fibroids lakini hakuna kitu
kilichothibitika moja kwa moja kuwa chanzo cha
fibroids. Kwa wale wenye uzito mkubwa
inashauriwa kupunguza mwili kunaweza
kupunguza uwezekano wa kupata fibroids.
Zipo tafiti zinazoonyesha kuwa matumizi ya
vidonge vya uzazi wa mpango vinapunguza
uwezekano wa kupata fibroids.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni