Kwenye mazoezi asubuhi ya leo,Tumba amepatwa na jeraha kubwa kwenye paji la uso lililomfanya kushonwa nyuzi tatu hapo hapo baada ya kugogwa kiwiko (kwa bahati mbaya) na nahodha Temi Felix walipokuwa wakiwania mpira.
Mkuu wa kitengo cha utabibu kwenye kikosini Dr Joshua Kaseko, amesema atatoa taarifa ya mwisho siku ya kesho kama mlinzi huyo atakuwa mmoja wa nyota watakaowakilisha City kwenye mchezo huo wa jumamosi.
“Tumemshona nyuzi tatu, taarifa ya yeye kucheza mchezo wa jumamosi nitaitoa kesho,hii ni kwa sababu nataka kutizama maendeleo yake ndani ya saa 24 zijazo,tukio hili limemsikitisha kila mtu lakini kwenye soka mambo haya hutokea, mimi pamoja na wenzangu(kitengo cha utabibu) tutajitahidi kuhakikisha anakuwa sawa tayari kwa mchezo huo kwa sababu mwalimu (Phiri) ameniambia kuwa anamuhitaji kama mtu muhimu kwenye safu ya ulinzi”, alisema.
Akiendelea zaidi Dr Kaseko amesema kuwa mlinzi wa kati Deo Julius aliyeumia kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi Tanzania Prison wiki mbili zilizopita anatarajia kuanza mazoezi jumatatu hii kufuatia kupona kwa majereha ya goti aliyokuwa ameyapata.
“Deo Julius sasa yuko tayari, ni uhakika kuwa ataanza mazoezi jumatatu, amekuwa nje kwa wiki mbili tukimuunguza majeraha ya goti, hili ni jambo jema kwetu kwa sababu kurejea kwake kikosini kunakuja kuimarisha safu yetu ya ulinzi alisema” Dr Kaseko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni