.

.

03 Machi 2016

UNAIKUMBUKA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA ANGANI MWAKA 2014? HABARI MPYA YAIBUKA


Kipande cha ndege kilichopatikana katika pwani ya Msumbiji kinaaminika kuwa cha Boeing 777, aina ya ndege ya Malaysia yenye nambari ya usajili MH370 iliyopotea miaka miwili iliyopita, Liow Tiong Lai, waziri wa uchukuzi wa Malaysia amesema.
"Ripoti za awali zinaonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kipande hicho kuwa cha ndege aina ya B777," Tiong Lai alisema.
Hata hivyo waziri huyo aliongeza kuwa uchunguzi zaidi unafanywa kuthibitisha uhusiano wa kipande hicho na ndege ya MH370.
Alisema kuwa maafisa wa usafiri wa ndege wa Malaysia kwa sasa wanashirikiana na wenzao wa Australia kuondoa kipande hicho kutoka kwenye bahari.
MH370 ilipotea tarehe nane mwezi Machi, 2014 ikiwa kwenye safari ya kuelekea Beijing kutoka Kuala Lumpur, Malaysia. Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 239 wengi wao wakiwa raia wa Uchina.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni