.

.

06 Juni 2016

MAKALLA AZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA WA MBEYA KUKAMILISHA ZOEZI LA UTENGENEZWAJI WA MADAWATI IFIKAPO JUNI 20 MWAKA HUU.

MAKALLA AZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA WA MBEYA KUKAMILISHA ZOEZI LA UTENGENEZWAJI WA MADAWATI IFIKAPO JUNI 20,AKATAA TAKWIMU HEWA ZA MADAWATI MBEYA,MADAWATI ASILIMIA 95 YAKAMILIKA-
Bado Siku kadhaa kutimia tarehe 30 juni hapa nchi kuhusiana na agizo alilotoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh.Dkt.John Pombe Magufuli kuhusu kukamilisha changamoto Ya Uhaba wa Madawati zoezi walilopewa Wakuu wa Mikoa hapa nchini.

Upande wa MKOA wa MBEYA tunakutana na Mkuu wa MKOA wa MBEYA Mh.Amos G.Makalla Leo katika ziara yake ya Kikazi wilayani Mbarali ameziagiza halmashauri zote za mkoa wa MBEYA kukamilisha utengenezaji wa Madawati ifikapo juni 20, na sambasamba na agizo hilo ametaadharisha juu ya takwimu za upungufu wa Madawati hewa kwa lengo la kuficha ukweli, Mh.Makalla ameyasema hayo Leo wilayani Mbarali wakati wa ziara ya kukagua utengenezaji wa Madawati na halfa ya kukabidhi Madawati 162 Katika shule ya Msingi Jangarutu.
Kwa takwimu Mkoa wa MBEYA una upungufu wa Madawati 32,000 na Mpaka sasa utengenezaji wa Madawati umefikia asilimia 95 na ametoa ahadi hadi tarehe 20 Juni kila Halmashauri iwe imekamilisha kuhusu udhibiti wa takwimu za Madawati hewa, ameagiza kila Mkuu wa Shule apokee Madawati kwa maandishi na yenye ubora kwa idadi ile ile iliyobainishwa awali kwa idadi kuwa ndiyo upungufu Madawati katika shule zao.
Amewataka wanafunzi na walimu kuyatunza Madawati wanayo kabidhiwa ili kutoa nafasi kwa Serikali ,Wadau, Wananchi , Kushughulikia changamoto zingine kama Ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa na Vyoo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni