.

.

30 Aprili 2015

NEPAL: KIJANA AOKOLEWA AKIWA HAI BAADA YA KUFUNIKWA NA KIFUSI KWA SIKU TANO NEPAL.


Kijana aliyeokolewa baada ya kufunikwa na kifusi kwa siku tano wakati wa tetemeko la ardhi mjini Kathmandu.
Kufuatia tetemeko kubwa la aridhi kuukumba Mji wa Kathmandu nchini Nepal siku tano zilizopita, waokoaji wamefanikiwa kumuokoa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 aliyepatikana hai baada ya kufunikwa na vifusi vya jengo alilokuwemo wakati wa tetemeko hilo.
Licha ya kuwa chini ya maporomoko ya vifusi hivyo kwa siku tano, taarifa zinasema kuwa kijana alisaidiwa na mwanya uliokuwa ukipenyeza hewa iliyomwezesha kupumua japo kwa shida.
Makundi ya watu walimshangilia alipotolewa huku akionekana akijitahidi kufungua macho yake. Alikimbizwa hospitali mara moja kupata matibabu zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni