.

.

24 Juni 2015

WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA WAVUTIWA NA ENEO LA VIWANDA


Kibao kinacho elekeza eneo la mradi wa viwanda wilayani Kisarawe mkoani Pwani lililopo Visegese. Mradi huo unaendeshwa na Halmshauri hiyo na wabia wa Kampuni ya World Map
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro (kushoto), akizungumza na viongozi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe,  Wabia wa eneo la mradi wa Kampuni ya World Map  na wawekezaji kutoka nchini China waliofika wilayani humo jana kuangalia fursa za kuwekeza viwanda katika eneo hilo. Kulia ni Ofisa Mipango Miji Mwandamizi kutoka TIC, Elibariki Ngorovily.
 Wawekezaji kutoka China wakiwa katika mkutano na uongozi wa wilaya ya Kisarawe na wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map kabla ya kwenda kuona eneo la mradi wa viwanda. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Makampuni ya Huallan 'Huallan Group', Tu Huobao, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo, Apple Ye, Huang Haitao na Meneja Masoko, Nara Zhou. (DK)
 Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoko (kulia), akizungumza katika mkutano huo wakati akiwakaribisha wawekezaji hao. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro,  Ofisa Mipango Miji Mwandamizi kutoka TIC, Elibariki Ngorovily, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Kigalu, Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Adam Ng'imba.
 Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Adam Ng'imba (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoko na Mkuu wa Wilaya hiyo, Subira Kigalu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni