Mbunge wa Moshi Vijijini na Mjumbe wa Nec ya CCM, Dk Cyrill Chami,
amewaomba walimu zaidi ya 2,700 wamuombee Waziri mkuu mstaafu, Edward
Lowassa, ili ‘ndoto’ yake iweze kutimia.
Staili hiyo mpya imekuja wakati CCM ikiwa imempiga ‘stopu’ kuendelea
na utaratibu wake wa kupokea makundi ya watu wanaomshawishi kugombea
urais na yeye (Lowassa) kuridhia na kuwaomba wananchi wasubiri
maelekezo ya CCM.
Marafiki hao ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Kilimanjaro,
walikwenda kitengo cha damu salama Kanda ya Kaskazini kuchangia damu
kama njia ya kutambua na kuenzi upendo wa Lowassa.
Tukio hilo la wanafunzi hao kwenda katika kitengo hicho,
kilitanguliwa na tukio la mkutano mkuu wa Chama cha Akiba na Mikopo
(Saccos) ya Walimu Moshi Vijijini kufanya mkutano wao mkuu. Katika
mkutano huo, Dk Chami aliyekuwa mgeni rasmi, aliwaambia amekwenda pale
akiwa na salamu kutoka kwa Lowassa kwamba anawapenda sana walimu.
“Anasema anawapenda na anawakumbuka sana na anawaomba mmuombee ili ndoto
yake na ile safari yake (bila kuitaja) itimie,” alisema Dk Chami na
walimu hao kulipuka kwa vigelegele.
Katika tukio la uchangiaji wa damu, wanafunzi zaidi ya 100 wa vyuo
vikuu mkoani Kilimanjaro, walitumia tukio hilo kumuunga mkono Lowassa
wakimsihi atangaze nia ya kuwania Urais 2015.
Mratibu wa marafiki wa Lowassa, Noel Nnko, alisema wanafunzi hao
wameamua kuchangia damu kumuunga mkono kada huyo kwa vile wao hawana
uwezo wa kutoa fedha za kuchangia fomu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni