KIKOSI
cha polisi usalama barabarani kimewataka madereva wa mabasi ,magari
makubwa pamoja na daladala kwenda kusoma ili kuongeza ujuzi wa kazi zao
kutokana na kuwepo kwa teknolojia za kisasa katika magari hayo.
Hayo
ameyasema,Ofisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,
Johansen Kahatano wakati wa semina ya kuwajengea uwezo madereva katika
kukabiliana na ajali za barabarani iliyofanyika jana katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam.
Alisema
sheria ya madeva wa mabasi ya abiria na magari makubwa kwenda
kujiendeleza kimasomo pamoja na kupata ujuzi kwa kila baada ya miaka
miwili pamoja na kupewa leseni mpya kwa sababu leseni zote zinakaribia
kuisha muda wake.
Kahatano,
alisema kuwa madereva wote wa malori wanatakiwa kusoma, kujikumbushia
vitu mbalimbali na kuongeza ujuzi wao kwa kila baada ya miaka 3,
ilikupunguza ajari za barabarani.
Katika
semina hiyo waendesha daladala wamesema kuwa kama serikali imeamua
madereva twende darasani tena, tunaomba gharama zote za mafuzo hayo
ziwe za waajili wetu au serikali.
CREDIT MICHUZI

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni