Kufuatia kauli ya Mbunge wa jimbo la mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu )kudai kuwa meya wa jiji hilo Atanasi Kapunga kuwa ametengeneza mikakati ya kuligawa jimbo la mbeya kwa maslahi yake binafsi nakwamba sababu zilizotolewa na meya huyo ni za kibabaishaji .
Akizungumza mjini Dodoma hii leo mbunge huyo amesema sababu za kibabaishaji za meya huyo juu ya wa ugawaji wa jimbo la mbeya mjini kwani ni sawa na kugawa moyo wake,
Kutokana na kauli hiyo msahiki meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, ameibuka na kudai kuwa hana sababu ya kuendelea kujibidhana na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi kwani amekuwa akimpa changamoto za kiutendaji ambazo zimemfanya kufanikiwa katika ufanisi wake wa kazi.
Amesema, Mbunge huyo anapaswa kusubili Tume ya uchaguzi itakapotoa kibali cha kuingia ulingoni kuliko kuendelea kulitumia Bunge kama sehemu ya kuwachafua watu ambao hawana nguvu ya kisheria ya kujibu tuhuma hizo Bungeni.
Akizungumza na blog hii Kapunga amesema , Sugu ni mjumbe wa vikao vya kiutendaji vya halmashauri ananafasi kubwa ya kufika na kuyazungumzia hayo tatizo linalomsumbua ni upeo wake mdogo wa kufikiri hivyo kujiaminisha kwamba Jimbo la Mbeya ni mali yake.
Alisema,Jimbo hilo ni la wananchi, si la ukoo na kitendo cha kuwaza jimbo ni mali yake ni ujinga, yeye atabaki kuwa kwenye horodha ya wabunge wa ajaabu ambao kila siku kazi yake ni kumuwaza Kapunga badala ya kusimama na hoja.
Amesema, wakazi wa Mkoa wa Mbeya ni watu ambao wameelimika hivyo hawapendi kudanganywa ni watu wanaojipenda na niwachapakazi hivyo majungu ya watu wachache hayawakatishi tama zaidi ni kufanya kazi.
Alisema, wananchi wanachotaka wao ni kiongozi bora na si kiongozi mbabaishaji , kiongozi anayetoa miongozo yenye maendeleo na misimamo.
Hata hivyo Kapunga alitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi kuhusu hali halisi ya utendaji kazi wake uliokuwa umezungukwa na majungu, chuki na fitina zisizokuwa na msingi zinazoendelea kutolewa na Mbunge Sugu aliyemfananisha na chipukizi wa kisiasa.
Amesema, majungu,fitina na chuki zilizokuwa zinatawala juu yake zimekuwa zikimsaidia kufanya kazi kwa bidii ili wale wote wanaoeneza ujinga akiwemo Sugu, waje kuonekana ni wapumbavu.
Amesema, mchakato wa kuligawa jimbo hilo, ulianza mwaka 2008 ukiwa chini ya Mbunge Mpesya hivyo yeye kama Meya ni jukumu lake kulisemeya hilo kama mtendaji wa halmashauri.
KUSIKILIZA SAUTI YA MEYA WA JIJI LA MBEYA
http://jamiimoja.blogspot.com/2015/05/meya-wa-jiji-la-mbeya-amjia-juu-mbunge.html#sthash.EcHLUAP7.dpuf
KUSIKILIZA SAUTI YA MEYA WA JIJI LA MBEYA
http://jamiimoja.blogspot.com/2015/05/meya-wa-jiji-la-mbeya-amjia-juu-mbunge.html#sthash.EcHLUAP7.dpuf
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni