Umoja wa mataifa unasema kuwa mapigano katika jimbo la Unity State nchini Sudan Kusini yamewaacha takriban raia 100,000 bila makao katika kipindi cha juma moja lililopita.
Mkuu wa umoja wa mataifa anayesimamia maswala ya binaadamu Toby Lanzer amevitaka vikosi vya serikali na waasi kuhakikisha kuwa hakuna raia atakayejeruhiwa wakati wa vita hivyo.
Bwana Lanzer amesema kuwa vijiji karibu na mji mkuu wa jimbo hilo Bentiu,vimeathirika zaidi na mapigano hayo.
Ameonya kuwa watu wamekuwa wakiyatoroka makaazi yao wakati wa msimu wa upanzi wakati ambapo wangekuwa wakipalilia mimea yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni