Ndugu zangu,
Jana
jioni pale Viwanja vya Furahisha Mwanza, tulionyeshwa kupitia runinga,
CCM ikiongozwa na Katibu wake Mkuu, Abdulhaman Kinana ikifanya mkutano
wa hadhara.
Ni tukio
la kuhitimisha ziara za kutembea nchi nzima ikiwamo wilaya, kata na
vijiji iliyofanywa na Abdulhaman Kinana na timu yake. Kuna niliyokuwa
nikiyatafakari wakati nikiangalia.
Nakiona
Chama Cha Mapinduzi kama kioo ambacho nchi nzima ndio inachokichukua
kujitazamia. Hata walio kwenye upinzani na CCM wanajitazama kupitia kioo
cha CCM. Si ajabu kabisa kuona hata walio kwenye upinzani wanatoa maoni
juu ya watangaza nia ya Urais kupitia CCM. Kwamba utasikia inasemwa
kutoka kwa wapinzani; kuwa fulani hafai, afadhali ya yule, ndani ya CCM!
Ingawa
kuna haja pia ya walio kwenye upinzani kutengeneza vioo vya kujitazamia,
lakini, hakuna ajabu ya wapinzania kujitazama kupitia kioo cha CCM.
Kiukweli CCM kuanzia TANU, si tu imekuwa madarakani muda wote, lakini,
ndio Chama kilichojenga misingi ya nchi hii. Hakuna ajabu basi, kuwa
hata ninapoandika fikra hizi. Vyama vya upinzani vinaisubiri CCM kwanza
itangaze mgombea wake Urais ndivyo navyo vifuatie.
Kimsingi,
CCM ni zaidi ya Chama cha Siasa. Ni taasisi kubwa na inayoongoza kwenye
nchi. CCM imebeba maslahi ya kina na mapana ya Watanzania zaidi ya
milioni 44. Katika hali tuliyo nayo sasa, CCM haipaswi hata kidogo,
kufanya maamuzi ya ovyo na ya kijinga yatakayoigharimu nchi hasara ya
miaka mingi.(P.T)
Katika
wakati tulio nao sasa, kama chama cha siasa kitataka kibaki kwenye
mamlaka ya uongozi kwa muda mrefu , na kwa kupitia masanduku ya kura,
basi, kina lazima ya kutafuta kuungwa mkono wa walio wengi kwa maana ya
watu.
Mwanafalsafa Benjamin Disrael anasema;
“ Mamlaka zote msingi wake ni imani, tunawajibika katika kuyatekeleza yaliyo kwenye mamlaka zetu, na kwamba, mamlaka yatatokana na watu, kwa ajili ya watu, na chemchem zote za fikra ziachwe hai”- Benjamin Disraeli.
Kwa kukiangalia anachosema Disraeli tunaona, kuwa kazi ya Chama ya cha siasa haipaswi kuwa ni kuudhibiti umma katika kuhoji yanayofanywa na Serikali, badala yake, Chama kinapaswa kuwa upande wa umma. Ni katika kuyaelewa mahitaji ya umma.
“ Mamlaka zote msingi wake ni imani, tunawajibika katika kuyatekeleza yaliyo kwenye mamlaka zetu, na kwamba, mamlaka yatatokana na watu, kwa ajili ya watu, na chemchem zote za fikra ziachwe hai”- Benjamin Disraeli.
Kwa kukiangalia anachosema Disraeli tunaona, kuwa kazi ya Chama ya cha siasa haipaswi kuwa ni kuudhibiti umma katika kuhoji yanayofanywa na Serikali, badala yake, Chama kinapaswa kuwa upande wa umma. Ni katika kuyaelewa mahitaji ya umma.
Na kwa
vile Serikali inapaswa kuwa mtekelezaji wa yale yaliyoamuliwa kwa niaba
ya umma, basi, kazi kubwa ya chama cha siasa ni kuisimamia Serikali
katika kuutekeleza wajibu wake huo. Na hapa tunaona ni moja ya kazi
iliyofanywa vema na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulhaman Kinana na timu yake.
Kinana hakujitanguliza yeye, alikitanguliza Chama kama nyenzo ya
kuwatetea wananchi kwa kuibana Serikali. Kinana na wenzake wamefanya
kazi ya kufuta vumbi la kwenye kioo cha CCM.
Ikumbukwe
pia, katika nchi, ustawi wa demokrasia na maendeleo ya kiuchumi
huimarika zaidi kwa kuwepo na uhuru wa kifikra. Kwamba uwepo wa tofauti
za kifikra si jambo baya, bali ni jema na la muhimu kwa maendeleo ya
nchi, kisiasa, kijamii na kiuchumi. Kwamba siku zote, mawazo na mahitaji
ya wananchi yatangulizwe.
Hivyo
basi, ustawi wa demokrasia na maendeleo ya kiuchumi huchangiwa pia na
uwepo wa wananchi wenye uwezo wa kutathmini michango itokanayo na
wengine katika jamii husika.
Ni muhimu
pia kukawepo kwa wanasiasa wenye uwezo wa kutathmini mambo na kuja na
hoja zenye mashiko kwa maslahi ya nchi, badala ya hoja zenye kulenga
kuibakisha nchi kwenye hali ya kugota kisiasa na kimaendeleo ya
kiuchumi.
Nasisitiza
hapa, uwepo wa siasa za vyama vingi ni jambo jema kwa nchi, lakini,
kukosekana kwa umakini katika kuendesha siasa za vyama vingi hupelekea
kupunguza ladha na maana ya kuwa na siasa za vyama vingi. Maana, vyama
vingi ina maana pia ya uwepo wa fikra nyingi zenye kutofautiana na hata
kufanana, lakini, ni vema zikawa ni zenye kujenga na kulinda maslahi ya
nchi.
Na hapa tulipo, CCM imekuwa ndio kioo cha nchi kujitazamia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni