Mhandisi katika Kampuni ya TSN Group, ambao ni wamiliki wa bohari
ya kuhifadhi mafuta ya TAPCO Mhandisi Michael Shimiu,(wa tatu kulia)
akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa
pili kushoto) na ujumbe wake wakati walipoitembelea Kampuni hiyo kuona
miundombinu ya kuhifadhi mafuta ya Kampuni hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa
wa Tanga Said Magalula na kulia ni Mkurugenzi wa TSN Group, Farouk
Baghoza.
Meneja Biashara sehemu ya Mafuta ya Petroli wa Kampuni ya Lake Gas, Jamal
Yahaya, akimwonesha Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene na
ujumbe wake, Matanki ya kuhifadhi gesi ya kampuni hiyo (hayapo pichani)
wakati Waziri alipotembelea kampuni hiyo mkoani Tanga.
Baadhi ya Matanki ya kuhifadhi mafuta ya kampuni ya TSN Group, wamiliki wa Bohari ya TAPCO.
Sehemu
ya wadau wa mafuta mkoa wa Tanga, wakifuatilia kikao baina ya Waziri wa
Nishati na Madini George Simbachawene, Uongozi wa Mkoa wa Tanga na
Taasisi za Serikali zinazosimamia masuala ya mafuta nchini.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Said, Magalula, akiongea jambo wakati wa kikao cha
majumuishi baina ya Mkoa wa tanga Wizara ya Nishati na Madini, Taasisi
za Serikali zinazohusika na masuala ya mafuta na wadau wa mafuta Mkoa wa
Tanga. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula na wa kwanza Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga, Mboni Mgaza.
Meneja
Mkuu wa PICL, Michael Mjinja (wa pili kulia), akiongea jambo wakati
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa tatu kushoto)
alipotembelea Bohari ya Kampuni ya GBP ya Tanga, kukagua miundombinu ya
kuhifadhi mafuta ya kampuni hiyo. Wa Pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Said Magalula,wa tatu kulia ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo
ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi, Hosea Mbise,
katikakati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni GBP ya Tanga, Badar
Masoud.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni GBP ya Tanga, Badar Masoud (katikati), akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, (kulia) kutembelea Bandari ya Tanga itakayotumika kwa katika shughuli za kushusha mafuta jijini humo. Wengine nyuma ni wadau wa Mafuta Tanga, na Uongozi wa Mkoa wa Tanga.
Waziri
wa Nishati na Madini George Simbachawene (wa pili kushoto) akikagua
miundombinu ya kuhifadhi mafuta katika Bohari ya Kampuni ya GBP ya
Tanga. Nyuma ya Waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula. Wengine
kutoka kulia ni Meneja Mkuu wa PICL, Michael Mjinja, Kamishna wa
Nishati na Maendeleo ya Petroli Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi,
Hosea Mbise na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GBP ya Tanga, Badar
Masoud. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa GBP, Bohari hiyo ina uwezo wa
kuhifadhi lita milioni 26 za mafuta.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bohari ya GBP ya Tanga, Badar Masoud akimwonesha akimweleza
jambo Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene wakati akikagua
miundombinu ya kuhifadhi mafuta katika Bohari ya Kampuni ya GBP , Tanga. Wengine katika picha ni Baadhi ya watendaji wa Wizara na wadau wa mafuta mKoa wa Tanga zikiwemo Taasisi za Serikali.
SIMBACHAWENE AKAGUA MIUNDOMBINU YA KUHIFADHI MAFUTA TANGA
Kufuatia
kuongezeka kwa kiwango cha mafuta yanayoingizwa nchini kupitia mfumo wa
Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja nchini (BPS), bandari ya Tanga itakua
bandari ya pili kupokea shehena ya mafuta kwa kutumia mfumo huo.
Hayo
yameleezwa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakati wa
kikao baina yake Uongozi wa Mkoa wa Tanga, Taasisi za Serikali
zinazoshughulika na masuala ya mafuta na wadau wa mafuta mkoani Tanga.
Aidha, Waziri alirejea kauli yake wakati akikagua miundombinu ya
kuhifadhi mafuta katika Bohari ya kampuni ya GBP na kampuni ya TSN group
wamiliki wa bohari ya TAPCO.
Akizitaja
faida za kutumia bandari hiyo ameeleza kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa
uhakika wa upatikanaji na usambazaji mafuta, kupunguza msongamano
uliopo kwa kutegemea Bandari ya Dar es Salaam, kupunguza gharama za
usambazaji mafuta ikiwemo kukuza uchumi wa Mkoa wa Tanga na hivyo
kuchangia zaidi katika Pato la taifa.
Akiongea
katika kikao hicho, Simbachawene amesema hiyo ni fursa nzuri kwa
serikali na itashirikiana vizuri na kwa kwa karibu na wadau wote walio
tayari kufanya kazi katika eneo hilo, na kuutaka mkoa huo kuipokea
shughuli hiyo kikamilifu kwani ni sehemu ya mafanikio ya mkoa huo.
“Kila
mdau anahusika katika suala hili, faida kwa Mkoa huu ni kubwa zaidi,
zipo faida za kiuchumi na kijamii, lakini pia usalama wa mafuta nchini,
mazingira ya sekta hii yamekua mazuri, ndio maana wenzetu jirani
wanapitia bandari ya Dar es Salaam, Tanga itasaidia zaidi katika
kufanikisha mafanikio haya”,ameongeza Simbachawene.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni