.

.

14 Julai 2015

HALI YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI DAR INATISHA


Wakati vijana 40,000 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24, wakibainika kuambukizwa ugonjwa wa Ukimwi jijini Dar es Salaam, viongozi, wabunge na wafanyabiashara wametajwa kuwa vinara wa kusambaza ugonjwa huo.
Mratibu wa Vijana wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Grace Kessy akizungumza katika warsha ya siku nne ya wawakilishi wa mashirika ya vijana yanayojihusisha na vita dhidi ya Ukimwi nchini jijini hapa alisema, vijana wasipobadili tabia wataendelea kuwapo hatarini.
Alisema katika taarifa zilizokusanywa mwaka 2011 hadi 2012 ilibainika kuwa, kati ya vijana waliopimwa 40,000 walikuwa na maambukizi Dar es Salaam, wakifuatiwa na vijana 10,000 kutoka mikoa ya Shinyanga, Kagera na Mbeya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni