.

.

06 Julai 2015

KOMANYA KUZIKWA JUMATANO



MAZISHI ya Askofu Mkuu na Mwanzilishi wa Kanisa la Cathedral of Joy (CoJ), Apostle John Komanya, yanatarajia kufanyika Jumatano, Julai 8, mwaka huu katika Makaburi ya Tabata-Segerea jijini Dar es Salaam.
Apostle Komanya alifariki dunia usiku wa kuamkia jana akiwa katika Hospitali ya Hindu Mandal, jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa.
Taarifa iliyotolewa ma mchungaji msaidizi wa kanisa hilo, Abel John Kigeli, ilieleza kuwa Apostle Komanya alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari pamoja na typhoid, na kwamba siku za nyuma alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo alikuja kuruhusiwa baada ya kupata nafuu.
Siku mbili nyuma ndipo alipozidiwa tena na hivyo kupelekwa Hospitali ya Hindu Mandal, ambapo mauti yalimkuta. Marehemu ameacha mke na watoto watatu ambao wako nchini Marekani, sehemu ambayo pia alikuwa akihudumu.
Kwa sasa msiba upo eneo la Tabata-Kisukulu, Dar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni