Mbunge wa Kasulu
Mjini ,Moses Machali amekihama rasmi chama hicho na kujiunga na ACT -
Wazalendo huku akiwaeleza wananchi waliofika kumsikiliza katika Uwanja
wa Shule ya Msingi Kiganamo mjini hapa kuwa hatasita kuachana na chama
chake kipya endapo kitaonekana kinatetea mafisadi na viongozi
wanaokandamiza demokrasia.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa kadi na kiongozi wa ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe,
Naibu Katibu Mkuu huyo wa NCCR - Mageuzi alisema amejiunga baada ya
viongozi wa chama hicho kumhujumu katika harakati zake za kutetea
masilahi ya Halmashauri ya Wilaya Kasulu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni