.

.

15 Julai 2015

Wasomi wetu wamegeuka vibogoyo

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salam, wakiwa nje ya Ukumbi wa Nkrumah uliopo kampasi kuu ya chuo hicho. Picha na Maktaba Ukipata fursa ya kuonana na kuongea na daktari bingwa yeyote wa magonjwa ya watoto au yule wa afya ya kinywa na meno, miongoni mwa ushauri mkubwa atakaokusisitizia ni ule wa kutowapa watoto wako vyakula vyenye sukari kwa wingi hasa biskuti, pipi au keki. Madhara yatokanayo na kuupuzia ushauri huu huwa ni kuoza kwa meno na hatimaye mtoto huyu kujikuta akiwa kibogoyo katika umri mdogo kabisa wa maisha yake. Mfumo wa elimu unaotumika kuwaandaa wasomi wetu nchini na barani Afrika kwa ujumla ni wazi kabisa umekuwa ukitengeneza vibogoyo kwa miaka nenda rudi. Kwa faida ya makala haya, kibogoyo ni mtu asiye na meno au kwa lugha rahisi mtu asiye na madhara kwa vitu vitamu kama nyama, mahindi ya kuchoma au karanga. Nchini Tanzania kijana hupitia mfumo wa elimu wa takribani miaka 16 mpaka kuwa mhitimu wa chuo kikuu. Huanza na miaka saba ya elimu ya msingi, miaka minne ya sekondari na mingine miwili ya sekondari ya juu na baadaye kuanza miaka mingine mitatu hadi mitano ya elimu ya juu.(

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni