UWEPO WA BABA WAKATI WA KUJIFUNGUA. Baadhi ya familia hawakubaliani nami kwamba ni vyema baba kuwepo katika tukio la kujifungua lakini kwakweli kwa maoni yangu ni vyema baba akashiriki kikamilifu yale mapenzi ya mama kwa mtoto. Kwanza inampa nguvu mama ajisikie kwamba hayuko pekeyake.Ni mda huu huwa nawahurumia akina mama wanaochukuwa mimba bila kujua ni nani kampatia mimba hiyo maana muda huu huwa wako peke yao na manesi wenye hila.
FURAHA YA BABA HUWA NI SAWA NA YA MAMA
Ni maumbile tu yanayo tofautisha furaha ya
mama na ile ya baba kwani ya baba uambatana na huruma kubwa sana na
ndiyo maana baadhi ya wababa hawapendi kuwepo kwenye tukio kwasababu ya
kutotaka kuona machungu anayo yapata mama.Na wengine wanashindwa kushika
kichanga kwani ukihurumia kwamba labda watakiumiza.Furaha ya baba na
mtoto ni sawa na ya mama na mtoto.Wapendwawasomaji,kuweni na christmas
njema na mwaka mpya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni