UNAHISI mwenzi wako anakusaliti kwa maana kwamba anafanya ngono na wanawake au wanaume wengine? Fahamu kuwa wapo wengi wenye kulalamikia hilo.
Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza kwanini hasa anatoka na wengine ikiwa aliahidi kwamba atakuwa ananipenda milele? Wengine wanakwenda mbali zaidi na kufikiri kila kitu ambacho anakifanya kwa mwenzi wake kitakuwa ni chenye kumpendeza mwingine.
“Mimi najitahidi kumfanyia mambo mengi mazuri, bado anaonekana haridhiki,” ndivyo baadhi ya watu wanavyojisemea.
UKWELI UKOJE?: Ni vizuri katika mapenzi kupata muda wa kuzungumza mwenzangu unapendelea nini na usingependa ufanyiwe nini.KUAMINI KUWA UNAYOFANYA NI MAZURI, BILA KUAMBIWA NA UNAYEMFANYIA, SIO SAHIHI.
Maisha ya raha katika uhusiano ni kuhakikisha kunakuwa na fursa ya wapendanao kukaa na kujadili namna gani wamekuwa wakiishi na nini cha kufanya ili waweze kuwa na maisha bora zaidi.
KUKWAZANA NI MAMBO YA KAWAIDA KATIKA MAPENZI. IKIWA UMEKAA KWENYE TUMBO LA MAMA YAKO NA BADO KUNA WAKATI MNAKWAZANA, IWE MTU AMBAYE MMEKUTANA TU MITAANI?Jambo muhimu katika ndoa ni kuhakikisha kunakuwa na nafasi ya wanandoa kujadili hali ya ndoa yao.
Kama ilivyo katika biashara kwamba wafanyabiashara wakati fulani wanajadili hali ya maendeleo ya biashara ili kujua kama kuna matatizo gani nk, ni muhimu sana wanandoa kutenga muda wa kujadili hali ya uhusiano wao.
SABABU ZA WATU KUSALITIWakati fulani nimekuwa nikiongea na watu wanaosaliti ndoa...baadhi yao ukiwauliza unaonaje sasa ukaondoa kwenye ndoa na kuoana na huyo wa nje, jibu ni kwamba hawezi kwa sababu anasaliti si kwa sababu hampendi aliyenaye, bali wakati mwingine ni kutofautiana.
Kwa mfano katika utafiti wangu nimegundua kwamba idadi kubwa ya wanandoa waume, hawana uhakika wa kupata tendo la ndoa kwa wakati wanaotaka, kama ilivyo kwa baadhi ya wanawake.
Tafiti ambazo nimekuwa nikifanya pia nimegundua kuna tofauti ya mahitaji katika ndoa, kwa mfano wakati wanaume ni wenye kuhitaji mno tendo la ndoa, furaha ya wanawake walio wengi sio hilo wakati fulani ni uhakika wa kupatikana kwa mahitaji ya ndani na amani.
*Kutopata mapenzi ya kweli katika ndoa hasa ikiwa Kijana/Binti alilazimishwa kuoa/kuolewa na mtu ambaye hakumpenda.-Wengine hawapata mapenzi ya kweli kwa sababu tu mwanaume au mwanamke hamjali, kitendo ambacho kinasababisha baadhi yao kuona kwamba suluhu pekee ni kwenda nje ya ndoa.
*Uchafu, kutojijali au kujipenda kwa mwanaume na mwanamke-Wapo wanaume na wanawake ambao wamekuwa wachafu wa mwili na kutojipenda, kiasi kwamba ukiwa nae unahisi kichefuchefu. Kuna wanaume na wanawake kwa mfano wanalala bila kuoga, wengine unakuta mwingine mlevi, mwingine hanywi, kisha anarudi nyumbani anaomba abusiwe...mhh! raha iko wapi hapa?*Kutotosheka/kuridhika katika tendo la ndoa
-Ingawa wakati mwingine huwa ni uroho wa mtu, mara nyingi hata majumbani watoto kama hawajashiba, baadhi yao hukimbilia kudowea chakula kwa jirani.
*Ubize wa kazi kupita kiasi/Kusafiri -Kuna watu wako bize kila kukicha, wakati mwingine si kweli kwamba wako bize bali ni unafiki au labda kutojua namna ya kupangilia mambo. Wengine ni watu wa safari kila mara, hiyo ni mbaya kwa wanandoa.
*Tamaa ya mali: Kuna wengine wako tayari kufanya ngono hovyo ili wapate mali. Huu ni ujinga, badala ya mtu kufanya kazi, anafikiri kwamba njia rahisi ni kubabaikia wanaume wenye magari, wenye fedha nk.
*Kujifunza mambo au mitindo mipya -Wakati mwingine kuna wengine wanatoka nje ili kusaka miondoka mipya...kuna wengine wamekuwa waoga wa kusema ukweli kwa wenzi wao juu ya yale ambayo wanayataka, matokeo yake wanaona wafanye hiyo ‘dawa mbadala’.
*Kutopata tendo la ndoa muda mrefu, labda kwa sababu mume ana matatizo au mke ana uja uzito mkubwa ama amejifungua n.k-Hata hivyo kitaalam kuna njia za kuridhishana si lazima tendo la ndoa la aina moja, bali wapenzi wanaweza kuchezeana na kila kitu kikawa chenye kuwafurahisha wote au kumfanya mwenzi wake afurahie.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni