Waziri
wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akipokea salamu wakati wa
ufungaji wa mafunzo kwa maofisa 27 wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi
za Taifa (TANAPA) ,mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani
Katavi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akikagua gwaride la
maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakati
wa kufunga mafunzo yao katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Maofisa
wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) wakila kiapo
cha utii wakati wa kumaliza mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika kambi ya
Mlele mkoani Katavi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akiwa na
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa TANAPA,Witness Shoo wakifuatilia
maonesho ya kijeshi kutoka kwa maofisa wa ngazi za juu wa shirika hilo
waliomaliza mafunzo katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe na wageni wengine waalikwa
wakiangalia umahiri wa maofisa wa Tanapa namna walivyopata mafunzo ya
kijeshi ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kutoka ule wa kiraia kwenda mfumo
wa jeshi Usu.
Maofisa
wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) waliomaliza
mafunzo ya kijeshi wakiwa wamebeba silaha kuonesha utayari katika
kupambana na ujangili katika Hifadhi za Taifa .
Maofisa
wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakionesha
umahiri katika kulenga Shabaha wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi kwa
maofisa hao yaliyofanyika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Waziri
wa maliasili na Utalii ,Prof Jumanne Maghembe akitizama matundu ya
risasi wakati wa zoezi la ulengaji shabaha kwa maofisa wa ngazi za juu
wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,mafunzo yaliyofanyika kambi la
Mlele mkoani Katavi.
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) Pascal Shelutete
akitoa muongozo wa namna wahitimu wa mafunzo hayo watakavyo pokea vyeti
mara baada ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) Allan Kijazi akizungumza
wakati wa kufunga mafunzo kwa maofisa wa ngazi za juu wa Shirika hilo
,mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Mkuu
wa wilaya ya Mlele ,Kanali Mstaafu ,Issa Njiku akizungumza wakati wa
kufunga mafunzo kwa maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za
Taifa (TANAPA) .
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa maofisa wa ngazi ya juu katika Shirika hilo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akitoa hotuba yake wakati
wa kufunga mafunzo ya kijeshi kwa maofisa wa ngazi ya juu wa Shirika la
Hifadhji za Taifa (TANAPA) mafunzo yaliyofanyika kambi ya Mlele mkoani
Katavi.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibooki
akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri Maghembe kufunga mafunzo
kwa maofisa wa ngazi za juu wa shirika hilo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii,Prof,Jumanne Maghemnbe akifurahia jambo na
maofisa wa ngazi ya juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,mafunzo
yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Maofisa
Uhifadhi wa ngazi ya juu katika Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA)
wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na
Utalii,Prof,Jumanne Maghembe mara baada ya kufunga mafunzo kwa maofisa
hao.
Maofisa
Uhifadhi wa ngazi ya juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi katika
kambi ya Mlele iliyoko mkoani Katavi.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni