.

.

16 Aprili 2015

MALAWI KUWAONDOA RAIA WAKE AFRIKA KUSINI


Raia wa kigeni wakijihifadhi vituo vya polisi kukimbia mashambulio yanayotokana na ghasia za kuwachukia wageni nchini Afrika Kusini

Malawi imesema itawaondoa raia wake kutoka Afrika Kusini kutokana na kuongezeka kwa ghasia za kuchukia wageni.
Watu wapatao watao, akiwemo mtoto wa miaka 14 wameuawa katika mashambulio ya kuwachukia wageni katika mji wa Durban nchini Afrika Kusini tangu wiki iliyopita.
Maduka mengi yanayomilikiwa na wageni katika jiji la Johannesburg yamefungwa kwa hofu ya kusambaa kwa ghasia.
Zimbabwe pia imeshutumu mashambulio hayo, ikiwalaumu wazalendo wa Afrika Kusini kwa kuwashambulia raia wa kigeni kwa madai kwamba wanachukua kazi zao.
Maelfu ya raia wa kigeni, hususan kutoka mataifa ya Afrika na Asia, walikwenda Afrika Kusini tangu utawala wa wazungu wachache ukome mwaka 1994
Watu wapatao 62 walikufa katika ghasia za kuchukia wageni zilizoikumba Afrika Kusini mwaka 2008.
Serikali ya Afrika Kusini imewaamuru polisi kuongeza nguvu katika kuwalinda raia wa kigeni.
Mpaka sasa Malawi ni nchi pekee iliyoamua kuwaondoa raia wake.
Waziri wa habari wa Malawi Kondwani Nankhumwa amesema kundi la kwanza litarejea nchini humo mwishoni ma wiki.
Raia wa Malawi wapatao 420 wameripotiwa kuishi katika kambi za wakimbizi mjini Durban baada ya kukimbia ghasia hizo.
Bwana Nankhumwa ameitaka AU na SADC kuingilia kati mgogoro huu ili kusaidia kuwalinda wageni.BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni