Pep Guardiola anatarajiwa kutua wiki ijayo na sasa swali kubwa lililopo ni je, atambakisha staa yupi? Pia wengi wanajiuliza iwapo ataendelea kumuamini Vincent Kompany kuwa nahodha wake na je, atafanya kazi tena na nahodha wa Ivory Coast.
Yaya Toure au atamuuza? Ikumbukwe Guardiola alifanya kazi na Toure kwenye klabu ya Barcelona, lakini akamuuza kuja City miaka mitano iliyopita na mchezaji huyo akaleta neema ya mataji Etihad. Hata hivyo, swali lisilo na majibu kwa sasa ni je, wawili hao watafanya kazi pamoja hasa ikizingatiwa kuwa, Tore kila mara amekuwa akilalamika kutoheshimiwa ndani ya klabu hiyo. Kama hiyo haitoshi,
Guardiola anasubiriwa kuamua hatima ya baadhi ya mastaa ambao mikataba yao inaelekea ukingoni huku baadhi yao umri pia ukianza kuwatupa mkono. Miongoni mwa mastaa ambao wanasubiri kocha huyo aamue hatma yao ni pamoja na kiungo Samir Nasri, beki Bacary Sagna, Wlfried Bony, Eliaquim Mangala na Aleksandar Kolarov. Wengine ni mshambuliaji wa Hispania, Jesus Navas, mlinzi wa kutegemewa wa Algentina, Pablo Zabaleta, Mfaransa Gael Clichy, Fabian Delph, Nicolas Otamendi, Fernando, Sergio Aguero na kipa anayetishia mara kadhaa kutaka kuondoka Joe Hart. Kikosi hicho ghali zaidi katika soka la Uingereza kilionekana kuwa tishio katika Ligi Kuu England kabla ya kuanza kwa msimu uliopita, lakini baadae kikaonekana si chochote wlolote baada ya kumaliza katika nafasi tatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni