RAIS Dk. John
Magufuli ameidhinisha kuwepo kwa wilaya tano katika jiji la Dar es
Salaam, badala ya tatu zilizokuwepo awali, ili kuleta maendeleo ya
haraka hususan katika elimu. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki,
alisema jana kuwa, waliwasilisha ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni
na Temeke kwa rais, ambapo ameshaliidhinisha.
“Hatua hii ya
kuwepo kwa wilaya tano italiwezesha jiji la Dar es Salaam, kupata
maendeleo ya haraka kwa kugawanywa kwa wilaya hizo, ambapo kutakuwa na
usimamizi thabiti na hakutakuwa na kisingizio cha kuelemewa kwa majukumu
kwa watendaji,”alisema.
Aliomba katika
ugawaji wa wilaya hizo, rasilimali zilizopo na mipaka igawanywe kwa
manufaa ya wananchi wa wilaya hizo. Aidha, alisema kinachosubiriwa ni
ugawaji wa mipaka na kutangazwa rasmi kuongezeka wilaya mbili ya
Kigamboni na Ubungo na kufi kisha idadi ya wilaya tano katika jiji la
Dar es Salaam.
Kutokana na
kuongezeka kwa wilaya, Sadiki aliwataka watendaji wake kuwa waadilifu
katika ugawaji wa mipaka na rasilimali zilizopo ili kuleta maendeleo
yaliyokusudiwa.
Akizungumzia
ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke, Sadiki alisema hadi
kufi kia jana, ombi hilo lilishaidhinishwa na rais, hivyo Kinondoni
itakuwa na wilaya mbili za Kinondoni na Ubungo huku wilaya ya Temeke
ikiwa na wilaya za Temeke na Kigamboni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni