Kenya leo imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya kimatifa ya wakimbizi.
Nchini Kenya sherehe za siku hii zimeandaliwa katika kambi kuu ya wakimbizi duniani ya Dadaab,pamoja na kambi ya Kakuma na vile vile jijini Nairobi.
Hata hivyo,sherehe
za mwaka huu zimeadhimishwa kwa huzuni miongoni mwa wakimbizi wanaoishi
Dadaab baada ya serikali kutekeleza agizo la kufunga kambi hiyo na
kuwaregesha Somalia
Hii ni baada ya kambi hiyo kutumika kama upenypo rahisi wa wanamgambo wa Alshabab.
Rais Uhuru Kenyatta amekutana na katibu wa umoja wa Mataifa wiki iliyopita aliyeunga mkono uamuzi wa Kenya lakini kutaka wakimbizi hao waregeshe kwa njia ya ubinadamu.
Waziri wa masuala ya mambo ya nchi za Kigeni Amina Mohammed amesema leo kwamba zoezi hilo linatekelezwa kwa utaratibu mzuri.
Asilimia 50 ya wakimbizi wa Dadaab hata hivyo hawangependa
kuregea Somalia.
Kambi ya Dadaab inamiliki zaidi ya wakimbizi laki tatu.
Imegeuka kuwa kitovu cha biashara ya thamani ya shilingi bilioni 2 kwa mwaka.
Kambi hii ina zaidi ya shule za msingi 46 na shule za upili 6 pamoja na vituo vya vya vyuo vikuu.
Licha ya kuwa wakimbizi wengi wanahofia kuregea kwao,baadhi yao kama Abdia Noor wanasubiri kwa hamu na ghamu kurudi kwao kwa familia zao baada ya kutengana nao kwa miaka mengi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni