.

.

12 Julai 2016

HISTORIA YA DAVID CAMERON KUIONGOZA UINGEREZA KUKAMILIKA JUMATANO






Baada ya Uingereza kupiga kura ya kujitoa Umoja wa Ulaya (EU) na hivyo Waziri Mkuu wa nchi hiyo, David Cameron kutangaza kujiuzuru kutokana na kushindwa kuwashawishi Waingerezza kusalia katika umoja huo, hatimaye Cameron ameitaja siku ya kuachia nafasi hiyo.

Cameron amesema kuwa Jumanne itakuwa siku yake ya mwisho kuhudhuria kabineti ya Uingereza na Jumatano itakuwa siku yake ya mwisho kuongoza Uingereza kama waziri mkuu.

Maamuzi ya Cameron kujiuzulu nafasi hiyo kumehitimisha miaka sita ya kiongozi huyo kuongoza Uingereza, nafasi ambayo alichukua kutoka kwa Gordon Brown mwaka 2010.

Aidha tayari mridhi wa nafasi yake ameshafahamika ambaye ni Theresia May ambaye amewaahidi wananchi wa Uingereza kujenga nchi imara na iliyo na mafanikio baada ya kujitoa EU.

Akimwelezea mridhi wake, Cameron amemtaja Theresia kuwa ni mtu ambaye hatetereki katika kufanya maamuzi na ni mshindani ambaye anaamini ataweza kutekeleza vyema madaraka yake ambayo atapatatiwa ya kuwa waziri mkuu wa Uingereza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni