.

.

03 Juni 2015

SUDAN KUSINI YAMTIMUA MJUMBE WA UMOJA WA MATAIFA.


Mbeyafm Redio's photo.

Sudan Kusini imeupinga wito wa Umoja wa Mataifa wa kuitaka ibatilishe uamuzi wake wa kumtimua mjumbe mkuu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa nchini humo. Nchi hio ilisema Toby Lanzer mratibu mkuu wa misaada ya kiutu wa Umoja huo, aliikosoa serikali mara kwa mara na kuwa alivuka mipaka kwa kusema serikali ya nchi hiyo inaelekea kuanguka
Msemaji Mkuu wa rais wa Sudan Kusini Ateny Wek Ateny, amezungumza kuwa ni vigumu kubadilisha uwamuzi wa kumfukuza nchi Toby Lanzer. Na kuongeza kuwa baraza la mawaziri lilitoa uwamuzi huo, baada ya kutathmini maoni ya mara kwa mara ya mjumbe huyo dhidi ya serikali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni