.

.

23 Machi 2016

STARS YAIBUKA NA USHINDI WA GOLI 1-0 DHIDI YA D'JAMENA YA NCHINI CHAD.





TANZANIA imepata ushindi wa kwanza katika Kundi G baada ya kuwafunga wenyeji, Chad 1-0 jioni hii Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya mjini hapa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani. 
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Jean-Jacques Ndala Ngambo, Aliyesaidiwa Na Olivier Safari Kabene na Nabina Blaise Sebutu wote wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Stars ilipata bao hilo kipindi cha kwanza.
Bao hilo lilifungwa na Nahodha Mbwana Ally Samatta aliyemlamba chenga beki Beadoum Monde baada ya kupokea krosi ya winga Farid Mussa na kufumua shuti lililomshinda kipa Diara Gerard.
Zikicheza katika jua kali la Alasiri, timu zote zilishindwa kucheza soka ya kuvutia na kushambulia moja kwa moja kutokana na nyasi bandia zilizochoka za Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya kuchakaa.
Pamoja na kufunga, Samatta alikosa mabao mawili ya wazi, wakati Thomas Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto nao pia walipoteza nafasi za kufunga.
Stars inaondoka kesho mchana mjini hapa katika ndege moja na Chad kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa marudiano Jumatatu Uwanja wa Taifa.
Kikosi cha Taifa Stars kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mwinyi Haji Mngwali, Erasto Nyoni, Kevin Yondani, Himid Mao, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/John Bocco dk46, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu/Ibrahim Hajib dk85 na Farid Mussa/David Mwantika dk73.
Chad; Diara Gerard, Abaya Cesar, Kevine Nicaise/Addassou Eli Mathieiu dk50, Nadjim Haroun, Beadoum Monde, Ndounnan Herman, Mahama Azarack, Betolgar Morgan, Djimenan Leger, Ndouassel Ezekiel Na Ninga Casimir.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni