.

.

27 Aprili 2016

MWAKATUNDU AMEREJEA KIKOSINI


IMG-20160420-WA0032
Kiungo wa Mbeya City fc Medson Mwakatundu aliyekuwaa akicheza kwa mkopo kwenye kikosi cha timu Geita Gold Sports ya Geita, amerejea  kujiunga na timu yake mara baada ya kumalizika kwa kipindi chake cha mkopo.
Akizungumza muda mfupi  baada ya  kuwasili kwenye kambi ya City akitokea  mkoani Geita, Mwakatundu anayecheza kwenye eneo la kiungo alisema kuwa anamshukuru mungu kurejea salama kutoka kwenye majukumu  kwa  timu ya Geita na sasa anafungua ukurasa mpya wa kuitumia timu yake.
“Nilijiunga na Geita Gold Sports kwa mkopo mwezi januari, Nimecheze mechi zote za  za ligi Daraja la kwanza na pia  mechi mbili za kombe la FA, nashukuru mungu nimerudi salama  sasa nawekea akili yangu  kwenye timu yangu, Nawashukuru viongozi na mashabiki wa timu ya Geita kwa ushirikiano wao, hakika wamefaanya kila jema kwangu na nimejifunza mengi  kutoka kwao”.
Kuhusu matokeoa ya mwisho wa michezo ya ligi daraja la kwanza kwa timu aliyokuwa akiitumikia, Mwakatundu alisema kuwa, ni viongozi wa Geita Gold pekee ndiyo wanaweza kulizungumzia  hilo jambo kwa sababu  yeye kama mchezaji majukumu yake yalikuwa uwanjani na anashukuru aliyatimiza asilimia 100.
IMG-20160420-WA0030
Medson Mwakatundu (kushoto).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni