.

.

02 Mei 2015

NDANDA FC WAZINDUKA, WAITUNGUA KAGERA SUGAR NANGWANDA, SASA WAITAKA YANGA

NDANDA FC wamefufua matumaini ya kubaki ligi kuu soka Tanzania bara baada ya jioni hii kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Wakata miwa wa Kagera Sugar kwenye mchezo uliopigwa Nangwanda Sijaona.
Goli  la kwanza la  Ndanda fc limefungwa na Dideon Benson dakika ya 15 na la pili limetiwa kambani na Nassor Kapamba dakika ya 45.
Mechi hiyo ambayo ambayo Ndanda walikuwa na uchu wa ushindi, Kagera Sugar wenye pointi 31 mpaka sasa hawakuonesha makeke kama walivyozelewa na kuwashangaza mashabiki waliojitokeza uwanjani.
‘Mtwara Kuchele’ Ndanda fc wamefikisha pointi 28 na angalau kufufua matumaini wakisubiri mechi ya Mei 9 mwaka huu dhidi ya Yanga.
Kocha msaidizi wa Ndanda fc, Ngawina Ngawina amesema mechi na Yanga ni ngumu lakini wanaisubiri kwa hamu ili kuwaonesha Watanzania uwezo waliokuwa nao.
Mechi ya kwanza uwanja wa Taifa, Yanga na Ndanda walitoka suluhu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni