Ajali za barabarani zimeendelea kupoteza maisha ya Watanzania ambapo leo asubuhi Mwendesha bajaji aliyejulikana kwa jina la Hussein Masha mkazi wa Nzega Ndogo wilayani Nzega mkoani Tabora amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Tipa.
Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Malunde1 blog kuwa mwendesha bajaji huyo alikuwa anatoka Nzega Ndogo kuelekea Nzega mjini ,alipofika katika eneo la Kitongo akataka kukata kona kuingia barabara ya posta ndipo tipa lililokuwa nyuma yake likagonga na kusababisha kifo chake papo hapo huku mwenye tipa akikimbia
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni