Ligi kuu ya England inakaribia kufikia tamati na jana Arsenal imeaonyesha nia ya kutaka kumaliza ligi hiyo ikiwa katika nafasi tatu za juu baada ya jana kucheza na Hull City.
Katika mchezo huo ambao Arsenal walionekana kuwadhibiti vyema wapinzani wao waliibuka na ushindi wa mabao 3-1, mabao ambayo yalifungwa na Alexis Sanchezamefunga mabao mawili, huku Aaron Ramsey akapachika moja na kuisaidia Arsenalkuibuka na ushindi huo dhidi ya wapinzani wao Hull City.
Kwa ushindi huo, Arsenal imeendelea kubaki katika nafasi ya tatu, ikiwa na pointi 70 sawa na Man City katika nafasi ya pili na imebakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni