.

.

09 Mei 2015

LIGI KUU TANZANIA BARA YAFIKIA TAMATI LEO, NIMEKUWEKEA HAPA TIMU ZILIZOSHUKA NA ZILIPONDA HAPA.


Pazia la ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2014/15 limefungwa rasmi leo, ambapo imeshudiwa timu za Ruvu Shooting na Polisi Moro zikishuka daraja baada ya kupoteza michezo yao.
Kwa kuanzia katika jiji la Mbeya, timu ya Mbeya City walikuwa wakiwakaribisha Maafande wa Polisi Moro ambao hata hivyo walikuwa tayari wameshuka daraja. Katika mchezo huo Mbeya City walishinda kwa bao 1-0.
Mkoani Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, kulikuwa na pambano kali na la kusisimua, ambapo Ndanda FC walikuwa wakiwakaribisha mabingwa wapya wa ligi hiyo Yanga SC na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0. Matokeo hayo yamezua shangwe na vifijo kwa Ndanda baada ya kijihakikishia nafsi yao ya kubaki ligi kuu kwani endapo wangepoteza mchezo huo basi wangeshuka daraja moja kwa moja.
Katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ilikuwa ni patashika nguo kuchanika pale Stand United walipokuwa awanawakaribisha Ruvu Shooting, matokeo ya mchezo huo ni kwamba Stand waliibuka na ushindi wa goli 1-0 kwa bila na kunusurika kushuka daraja, huku Ruvu Shooting wao wakiteremka daraja.
Huko Manungu Complex katikati ya mshamba ya miwa, Mtibwa walikuwa wakiwakaribisha Wagosi wa Kaya Coastal Union, ilishuhudiwa timu hizo zikitoshana nguvu kwa kufungana goli 1-1 na hata hivyo timu hizo kusalia katika ligi kuu msimu ujo.
Nao Tanzania Prisons ya Mbeya na Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera walitoshana nguvu kwa kutoka suluhu, mchezo huo ulipigwa katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza. Matokeo hayo yameinusuru Prisons kushuka daraja na kusalia ligi kuu kwa msimu ujao.
Nako katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, timu ya JKT walikuwa wanawakaribisha Wekundu wa Msimbazi Simba Sc na kushuhudia Simba wakiibuka na ushinda wa magoli 2-1. Mchezo huo ulikuwa hauna athari yoyote kwa timu zote mbili, hivyo kusalia ligi kuu.
Kwenya uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Azam Fc waliwakaribisha vijana wa Mgambo JKT kutoka jijini Tanga na kushuhudia timu hizo zikitoka suluhu.
Timu ambazo zimepanda ligi kuu kwa msimu ujao ni Mwadui FC, Majimaji, Toto Africans na African Sports.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni