Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Ndugu juma Khatibu Chum
amewataka wananchi wa Mkoa wa Morogoro kujiandikisha kwenye daftari la
wapiga kura ili kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi kwenye
uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Juma Khatibu
ameyasema hayo leo wakati akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru katika uwanja
wa mkesha wa mwenge eneo la Kichangani katika Tarafa ya Tuliani
Wilayani MvomeroMkoani Morogoro.
Amesema mwananchi yeyote ambaye
amefikisha umri wa mika 18 na mwenye sifa zote za kuandikishwa aende
kujiandikisha ili aweze kupata fursa ya kuchagua viongozi bora
watakaoiongozi nchi katika Serikali ya awamu ya tano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni