.

.

16 Juni 2015

BABA ADAIWA KUMBAKA MWANAWE, ALAZWA ICU


Mtoto wa miaka 10 (jina limehifadhiwa), anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Mapinduzi mjini Shinyanga, anadaiwa kubakwa na baba yake wa kambo na kusababisha kulazwa katika chumba cha wagonjwa chini ya uangalizi maalum (ICU) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kwa mujibu wa Mama wa mtoto huyo, alisema tukio hilo lilitokea Juni 13, mwaka huu, asubuhi baada ya yeye (mama) kwenda katika biashara zake za kuuza matango na kumuacha mume wake, nyumbani na mtoto huyo. Hata hivyo, alisema muda mfupi baadaye alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanawe amebakwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni