![]() |
Wafanyakazi wa uokoaji wakiwa karibu na eneo ilipozama meli
|
Waziri wa Usafirishaji wa China amesema
wafanyakazi wa vikosi vya uokoaji wanafanya kila jitihada kuhakikisha
wanawapata watu walionusurika miongoni mwa mamia ya waliokumbwa na mkasa wa
kuzama kwa meli katika mto Yangtze kutokana na hali mbaya ya hewa.
Maelfu ya waokoaji walifanya kazi usiku kucha
katika meli hiyo iliyopinduka ijulikanayo kama "Nyota ya Mashariki"
katika jimbo la Hubei.
Watu saba wamethibitika kufa na wengine 14
wamekutwa hai katika meli hiyo iliyokuwa na watu 456.
Ndugu waliojawa na hasira wanalalamikia
kukosekana kwa taarifa za uokoaji.
Watu walionusurika ni pamoja na nahodha wa
meli na mhandisi mkuu, wote wawili wakiwa katika mahabusu za polisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni