Jamal Malinzi, akisisitiza jambo wakati wa hafla hiyo.
Muonekano wa jezi mpya ya nyumbani.
Muonekano wa jezi mpya ya ugenini.
……………………………………………………
Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa, zitakazokuwa
zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali itakayokua
inazikabili.
Uzinduzi huo wa jezi mpya
uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la Golden Jubilee
uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho, uliongozwa na mgeni
rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.
Katika uzinduzi huo, kulizunduliwa
jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini, jezi za nyumbani na jezi
zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.
Ifuatayo ni hotuba ya Rais wa TFF ,
Jamal Malinzi aliyoisoma wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za timu za
Taifa, uzinduzi wa tovuti mpya ya TFF na kutunuku vyeti kwa viongozi
mbalimbali, makocha, wachezaji na wadhamini.
Mh Said Mtanda Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
Mzee Said el Maamry Mwenyekiti Msataafu wa FAT
Ndugu Leodeger Tenga Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF na Rais mstaafu wa TFF
Ndugu wageni waalikwa
Ndugu waandishi wa habari
Mabibi na mabwana
Salam aleikum.
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi
Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha hapa leo na kwa mafanikio mbali
mbali ambayo tumekuwa tukiyapata.Ninakushukuru sana ndugu mgeni rasmi
kwa kuacha shughuli zako kuja kujiunga nasi asubuhi hii katika shughuli
hii.
Ndugu mgeni rasmi,tarehe 08 oktoba
1964 Tanzania ilipata uanachama rasmi wa shirikisho la mpira wa miguu
duniani FIFA. TFF tuliona jambo zito kama hili hatuwezi kuliacha lipite
hivi hivi.Hivyo mwaka jana tuliamua kuenzi maadhimisho ya miaka 50 ya
kujiunga na FIFA kwa kufanya mambo mambo matatu makubwa.
La kwanza ni kutoa vyeti maalum
kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali kwa kutambua mchango wao
uliotukuka katika kuendeleza mpira wa miguu Tanzania.
Leo hii ndugu mgeni rasmi
tutakuomba ukabidhi vyeti hivi kwa wawakilishi wa makundi kadhaa kwa
niaba ya wenzao.Makundi haya ni pamoja na viongozi wa kitaifa
wastaafu,mawaziri wa michezo wastaafu,viongozi waliopita wa TFF?
FAT,wakurugenzi wa idara ya
michezo,wenyeviti na makatibu wa baraza la michezo la taifa,Timuya Taifa
iliyocheza fainali za Afrika mwaka 1980,waamuzi,makocha,wachezaji wa
timu ya Taifa na watangazaji mahiri wa michezo.Jumla tumetunuku vyeti
194.
Kiuhalisia idadi hii ni ndogo sana
ukilinganisha na wingi na uzito wa michango ya wadau mbali mbali wa
mpira katika miaka 50 iliyopita.
Tunaomba Watanzania wenzetu
watuelewe katika hili kuwa hawa tutakaowatunuku vyeti hivi ni
wawakalilisha wa wadau wote wa mpira Tanzania.
Ninaomba tusimame kwa muda mfupi
tuwaombe ewadau wenzetu na viongozi wa mpira wa miguu ambao wako katika
orodha hii na wametangulia mbele ya haki.
Ndugu mgeni rasmi katika kuenzi
miaka 50 ya Tanzania kujiunga na FIFA leo hii pia tutatoa mchango wa
fedha kwa makundi yenye mahitaji katika jamii.
Pesa hizi zinatokana na makusanyo
mbali mbali ikiwemo makusanyo ya mechi ya ngao ya hisani ifanyikayo kila
mwaka. Makundi haya ni pamoja na walemavu wa viuongo,walemavu wa ngozi
na wasioona.
Kitendo hii ni moja ya juhudi za
TFF kurudisha katika jamii kile tunachokusanya. Kila kundi litapewa
shilingi milioni tano na tunaendelea kupokea maombi toka makundi mbali
ya kijamii na tukiyapitisha tutaendelea kugawa fedha hizi.
Jambo la tatu tutakalolifanya leo litakuwa ni kuzindua rasmi tovuti mpya ya TFF (www.tff.or.tz).
Tumeamua kufanya jamabo hili katika kuenzi miaka hamsini ya kujiunga na
FIFA ili kutoa msisitizo kuwa sasa TFF na sisi tunajiunga Na kuendeleza
mpira kisasa kulingana na teknolojia iliyopo.
Kupitia tovuti hii wadau wa mpira
watapata fursa ya kuhabarishwana kuelimishwa nkuhusu masuala mbali mbali
yahusuyo mpira wa miguu.
Tovuti hii itakuwa pia na sehemu
ya kumbu kumbu (archive) zihusuzo historia ya mpira wa miguu na matukio
mbali mbali katika historia ya mpira wetu.
Tunaomba wadau wenye kumbu kumbu
mbali za mpira kama picha,takwimu,vipande vya magazeti ya zamani na
kadhalika mtuletee ili viingizwe katika tovuti yetu.
Tunaamini tovuti hii itakuwa ndio chanzo kikuu cha taarifa na rekodi mbali mbali za sasa na za zamani zihusuzo mpira wa miguu.
Ndugu mgeni rasmi shughuli ya leo
tutaihitimisha kwa kuzindua jezi mpya ya timu ya Taifa. Jezi hizi
zitakuwa ni mbili moja ya ugenini na nyingine ya nyumbani.Tunawapongeza
watanzania wote walioshiriki katika kubuni jezi na mwisho tuliunganisha
ubunifu tofauti na kupata jezi itakayozinduliwa leo.
Ubunifu huu tayari umetafutiwa
hati miliki Brela hivyo TFF tutalinda hakii hii kwa kuwakamata na
kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote watakaodiriki
kuchapisha na kuuza kwa magendo jezi hizi.Utaratibu unafanyika kumpata
msambaji mmoja halali atakayesambaza jezi hizi nchini kwa ajili ya
wapenzi wa mpira wa miguu.Ukinunua jezi hii utakuwa umechangia maendeleo
ya mpira wa miguu.
TFF inawashukuru na kuwapongeza
sana Tanzania Breweries ltd ambao ndio wazalishaji wa bia ya Kilimanjaro
Lager kwa sapoti wanayoitia kwa timu ya Taifa na kutuwezesha kubuni na
kuzalisha jezi hizi.Tunawashukuru sana.
Ndugu mgeni rasmi ninaomba
nimalizie kwa kuzungumzia kwa kifupi program yetu ya mpira wa vijana.kwa
kutambua umuhimu wa kuendeleza soka la vijana TFF tumejipanga vilivyo
kwa mpambano wa hatua za awali za kucheza fainali za vijana za Afrika
umri chini ya miaka 17 mwaka 2017.
Mechi za ufaulu zitafanyika kati
kati ya mwaka 2016.TFF tayari tumeunda kikosi cha awali cha vijana chini
ya umri wa miaka 15 kujiandaa na michuano hii.Kikosi hiki kimetokana na
michuano ya copa coca cola ya mwaka jana.
Tunapenda tuchukue fursa hii
kumshukuru Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha nchi yetu ya
Tanzania,kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii,kupata uenyeji
wa fainali za Afrika. Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF limeipatia
Tanzania uenyeji wa fainali za Afrika za vijana umri chini ya miaka 17
mwaka 2019.
Tunaomba Serikali itushike mkono
katika hili ili tuweze kuandaa mashindano mazuri.Lakini haitakuwa vyema
Tanzania kuandaa mashindano mazuri lakini tukatolewa hatua ya
makundi.Siku ya jumapili tarehe 07/juni TFF tutazindua mashindano ya
taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 mjini mwanza.
Wachezaji bora wa mashindano haya
ndio wataunda kikosi cha awali cha Taifa kwa ajili ya kushiriki fainali
za Afrika watoto umri chini ya miaka 17 mwaka 2109.
Tunaomba Serikali pamoja na wadau wote tushirikiane katika kukilea kikosi hiki ili mwaka 2019 tuwe na timu nzuri.
Tunamshukuru Mh Dr Fennela
Mukangara na wizara nzima ya habari vijana utamaduni na michezo kwa
ushirikiano wanaotupatia katika hatua hizi na katika shughuli nyingine
za kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu.
Ndugu mgeni rasmi ninaomba sasa nikukaribishe uhutubie hafla hii na pia utuongoze katika shughuli zitakazofuata.
Ahsate sana
Jamal Malinzi
Dar es salaam
03/juni/2015
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni