.

.

27 Julai 2015

AJALI YA TRENI YAUA WANNE TABORA

Watu wanne wamefariki papo hapo na wengine zaidi ya arobaini kujeruhiwa baada ya Treni ya mizigo,kuligonga basi kampuni ya Don’t Worry lililokuwa likitokea mjini Tabora kuelekea ufuruma  uyui mkoani humo  lilipofika eneo la kuvuko cha reli eneo loa malolo manispaa ya Tabora katika kile kilichodaiwa kuwa ni uzembe wa dereva.
Mashuhuda wa ajali hiyo  wamesema kuwa, dereva aliyekuwa katika mwendo wa kasi alitaka kukatiza haraka bila kuzingatia eneo hilo inapopita Treini hata kama aliiona Treini hiyo, na ndipo alipokata kona ya ghafla na basi hilo kuanguka kwenye reli na Treini kuigonga na kukutoa paa lote la juu la gari.
 
Aidha kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora  kamishina msaidizi Juma Bwire amesema kuwa katika ajali hiyo ya basi lenye namba za usajili T568 ABP,wanaume watatu na mwanamke mmoja wamepoteza maisha huku dereva aliyejulikana kwa jina la Kaonjo Iddy (34) akitoroka baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo majeruhu wamepelekwa katika hospitali ya rufaa na mkoa wa Tabora.
 
Viongozi wa shirika la reli waliofika  katika eneo la ajali hiyo wamesema kuwa madereva hawazingatii usalama wa barabarani kwani shirika la reli limejitahidi kuhakikisha linaweka alama husika lakini kutokana na mazoea mabaya hawajali na matokeo ni kusababisha ajali mbaya kama hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni