Wakati
vuguvugu la uchaguzi mkuu wa rais,wabunge na madiwani likiendelea kwa
kasi mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha demokrasi na mendeleo
chadema Bi.Chiku Abwao amejitoa katika chama hicho na kujiunga rasmi na
chama cha ACT wazalendo.
Bi.Abwao amesema ameridhishwa na uongozi wa ACT-wazalendo, katiba
na ilani ya uchaguzi wa chama hicho hadi kumpelekea kuamua kujiunga kwa
vile kinalenga kumkomboa mtanzania masikini pamoja na kuweka msingi
imara ya maadili ya viongozi.
Awali akizungumza kwa niaba ya katibu mkuu wa ACT-wazalendo, katibu
wa mipango na mikakati Bwana Mchanga Habibu amesema chama cha
ACT-wazalendo kimepata maendeleo makubwa kwa muda mfupi kutokana na kuwa
katiba bora, kufuata azimio la Tabora na ilani ya uchaguzi iliyobora
hali inayochangia wanasiasa wengi kujiunga na ACT kwa kuwa ndio chama
kinacholenga kuwakomboa wananchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni