BAADA ya vuta
nikuvute katika vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), kuhusu kukubaliwa au kutokubaliwa kwa Waziri Mkuu Mstaafu,
Edward Ngoyai Lowassa kujiunga na umoja huo ili kuongeza nguvu ya
kisiasa, hatimaye mwanasiasa huyo maarufu nchini amekubaliwa na tayari
amejiunga rasmi Ukawa akiwa mwanachama halisi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), imefahamika.
Taarifa rasmi
kutoka Ukawa na kwa msemaji wa Lowassa ambaye hakutaka jina lake
litajwe, imeeleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya majadiliano ya kina
katika Mkutano Mkuu wa Ukawa uliofanyika mapema wiki hii huku ajenda
kubwa ikiwa ni kumpokea Lowassa ili kuimarisha kambi ya upinzani ikiwa
ni pamoja na kumsimamisha kama mgombea urais wa umoja huo.
Taarifa rasmi
zimeeleza kuwa Lowassa anatarajiwa kutangazwa rasmi Jumapili hii hivyo
maadalizi ya mkutano mkubwa wa aina yake yanaendelea. Chanzo chetu
kutoka katika mkutano huo kilisema kwa moyo mmoja, wenyeviti wa vyama
vyote vinavyounda umoja huo, yaani Freeman Mbowe (Chadema), Profesa
Ibrahim Lipumba
(CUF), James Mbatia (NCCRMageuzi) na Emmanuel Makaidi (NLD), wameridhia
kuungana na Lowassa katika safari yao ya kuking’oa CCM madarakani huku
wakiamini kuwa wakimsimamisha kuwa mgombea wa Ukawa watafanikisha azma
ya vyama vya upinzani kuingia ikulu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni