.
08 Julai 2015
HAWA NDIO WACHEZAJI 10 WALIOONDOKA KIKOSI CHA MBEYA CITY FC AMBAO WALIKUWEPO MSIMU ULIOPITA NA MSIMU HUU WA 2015/2016 HAWATAKUWEPO.
Nyota 10 waliokuwa sehemu ya kikosi cha Mbeya City Fc msimu uliopita, rasmi hawatakuwepo msimu mpya wa 2015/16 unaotarajia kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi ujao.
Kwa mujibu wa Meneja usajiri wa City, Frank Mfundo, wachezaji hao 10 ambao hawatakuwepo City wanatangulia idadi nyingine ya watakaoachwa mara baada ya mazungumzo kati yao na klabu kukamilika mwishoni mwa juma hili.
“Kwenye kikosi cha City msimu huu, Paul Nonga,Deus Kaseke,Peter Mwalyanzi, Peter Mapunda,Fredy Cosmas,Idrisa Rashird,Lambony Luvanda Ashery,David Burhani, Anthony Matogolo na Deo Julius hawatakuwepo, hii ina maana kuwa wameachwa, hii ni kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuisha mikataba na hakukuwa na mazungumzo yoyote juu ya mikataba mipya huku wengine kati yao wakiwa tayai wamejiunga na timu zingine”
alisema Mfundo.
Katika hatua nyingine Mfundo amedokeza kuwa kuna wachezaji wengine kadhaa ambao bado wako kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu hivyo taarifa ya mustakabali wao ndani ya kikosi cha City itatolewa mwishoni mwa juma hili mara baada ya mazungumzo kukamilika.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni