Kamanda
wa jeshi la polisi wa mji wa Johar nchini Somalia ametangaza kuwa watu
50 wametiwa mbaroni wakishukiwa kuwa na uhusiano na kundi la al Shabab.
Sayad
Ndje ameashiria vitisho vya kundi la al Shabab na kueleza kuwa, watu 50
wametiwa mbaroni wakishukiwa kuwa na uhusiano na kundi hilo. Watu hao
wamekamatwa katika operesheni ya pamoja iliyofanywa na vikosi vya
usalama vya Somalia na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika
katika mji wa Johar kwenye mkoa wa Shabelle ya Kati, huko kusini mwa
Somalia.
Kamanda
wa polisi wa mji wa Johar ameongeza kuwa vikosi vya usalama vya Somalia
hivi sasa vimeimarisha usalama huko Shabelle ya Kati kwa kuzingatia
kuweko wawakilishi wa gazi ya juu wa makundi mbalimbali ambao
wanashiriki mkutano unaojadili kuundwa serikali mpya katika mkoa huo.
Kundi la
al Shabab ambalo limepoteza maeneo mengi yaliyokuwa chini ya udhibiti
wake, lingali linaendeleza mashambulizi yake nchini Somalia na katika
nchi jirani ya Kenya.
Credit http://www.mjengwablog.com/
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni