Mkazi wa
Shikombe wilayani Geita, Buhula Ngassa (47) amekamatwa na vitambulisho
43 vya wapiga kura, hata hivyo amedai vilikuwa vya wateja wake waliofika
kwake kusajili simu.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Geita, Joseph Konyo amesema leo kuwa mtuhumiwa Ngassa
alikutwa na vitambulisho vya zamani 7 na 36 ni vipya ambavyo
vitengenezwa kwa kutumia teknolojia ya BVR.
Kamanda Konyo
ameongeza mtuhumiwa amejitetea kuwa vitambulisho hivyo vilikuwa ni kwa
ajili ya kuwasajilia wateja waliofika kwake wakihitahitaji huduma hiyo
hivyo alikuwa anaenda maeneo ya mjini ili avidurufu na kupata kumbukumbu
atakazoziwasilisha kwa kampuni za simu.
Hata hivyo RPC
Konyo amesema uchunguzi zaidi unaendelea kubaini ukweli wa sakata hilo.
Awali, ilidaiwa kuwa mtuhumiwa alikamatwa na vitambulisho 200 vya kura
lakini Jeshi la Polisi Geita limethibitisha kuwa ni 43 pekee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni