Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) lipo katika mchakato wa mwisho wa kuanzisha kampuni
ya kutengeneza nguzo za umeme za zege, ikiwa ni mkakati wa uboreshaji
huduma kwa wateja wake, kupunguza matumizi ya nguzo za miti na kudhibiti
uharibifu wa miundombinu hiyo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba
(pichani), alisema kampuni hiyo ambayo itakuwa chini ya shirika hilo
inatarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa mwaka huu mchakato wa kuisajili kwa
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) utakapo kamilika.
Alisema hatua ya
shirika hilo kuanza kutumia nguzo za zege badala ya za miti ni moja ya
mikakati ya shirika ilo kuhakikisha linatoa huduma bora na za uhakika
kwa wateja wake kwani mara nyingi nguzo za miti zimekuwa hazidumu na
kulazimika kubadilishwa mara kwa mara kutokana na uchakavu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni