.

.

23 Julai 2015

MASHINE ZA BVR ZAZIDI KUHARIBIKA DAR ES SALAAM

Zoezi la uandikishaji wananchi kwa kutumia mfumo wa kielectronic jijini Dar es Salaam bado linaendelea kwa kusuasua huku mashine nyingi zikishindwa kufanya kazi.
Ni moja ya mashine ya kuandikishia wananchi maarufu kama BVR ikiwa dhoofu bin hali baada ya kushindwa kufanya kazi ikiwa ni dakika 30 pekee tangu kufunguliwa kwa kituo huku maafisa wa tume wakisema imeishiwa umeme.
 
Zaidi ya vituo 23 vya kuandikishia vilivyozungukiwa na waandishi wa habari ndani ya manispaa ya Temeke ikiwa ni siku ya pili ya zoezi la uandikishaji, mashine za BVR moja hadi mbili katika kila kituo zilikuwa ni mbovu, huku waathirika wakuu wakiwa ni akinamama waliofika kujiandikisha na watoto wao.
 
Licha ya tume ya taifa ya uchaguzi kujinasibu kupitia mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kusema hakutakuwa na changamoto zozote za kiuandikishaji bado inaonekana dhahili maafisa wa tume hawana uwezo wa kutumia mashine za BVR.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni