Chama kikuu cha upinzani cha Uingereza cha Labour kimemchagua kiongozi mpya, Jeremy Corbyn, wa siasa za mrengo wa kushoto.
Alishinda kwa kishindo ingawa alipoanza hakufikiriwa kabisa kuwa atafikia uongozi.
Corbyn ameongoza katika kampeni akiwa na ajenda ya mabadiliko makubwa, pamoja na azma ya kutaifisha tena sekta fulani za uchumi.
Mapendekezo
yake yamepokewa vema na wale waliochoka na sera za kubana matumizi, na
kile wanachoona kuwa wanasiasa wakuu wasiofahamu hali ya mtu wa kawaida.
Wagombea wengine watatu walitaka chama cha Labour kibaki katika siasa za wastani.
Katika
hotuba yake baada ya kuchaguliwa, Bwana Corbyn alilaani kile alichosema
ni tofauti ya kuchusha baina ya matajiri na mskini.
Alisema nchama chake kina umoja na kimeazimia kuleta jamii inayoheshimika na njema zaidi,CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni