Uchunguzi unaendelea baada ya picha ya ngono kuonyeshwa katika televisheni wakati wa maombolezi ya baba na mwanawe.
Ibada ya Simon Lewis mwenye umri wa miaka 33 na mwanawe ilifanyika
katika eneo la kuchoma maiti la Cardiff Thornhill siku ya Jumatano
Kiongozi wa ibada hiyo Lionel Fanthorpe alisema kwamba kisa hicho
kiliwaacha waombolezaji wakiwa wamekasirika na mamlaka ya Cardif ikaomba
msamaha kwa familia kwa kisa hicho kisicho cha heshima.
Bwana Lewis na mwanawe walifariki kufuatia ajali mjini Cardif katika siku ya mkesha wa mwaka mpya.
Chombo cha habari cha Media Wale kiliripoti madai kutoka kwa
muombolezaji ambaye hakutaka jina lake lijulikane kwamba picha za ngono
zilionekana katika runinga hiyo.
Runinga nne zilitumika kuonyesha
risala za rambi rambi na baraza hili lilisema kuwa televisheni
ilioonyesha picha hizo chafu ilikuwa imewekwa hivi majuzi.
''Tunajaribu kubaini iwapo runinga hiyo mpya ambayo ni aina ya smart tv
huenda ilinasa picha hizo kwa bahati mbaya kupitia bluetooth ama kupitia
wavu wa Wi-fi,''alisema msemaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni