Madereva wa daladala zinazofanya safari zake kati ya Uyole, Isyesye
na Ituha uelekea maeneo ya Majengo na Stendi kuu jijini Mbeya leo
wamefanya mgomo ambao umeambatana na vurugu kubwa wakipinga kupita
kwenye barabara kadhaa ambazo wamepangiwa na Sumatra kwa madai kuwa
barabara hizo ni mbovu na hazina vituo vya kupakia na kushusha abiria.
Kutokana na vurugu hizo jeshi la polisi limeamua kuingilia kati kwa
kuwatawanya madereva hao kwa mabomu ya machozi na akizungumzia mgomo
huo, kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, kamishna msadizi mwandamizi wa
jeshi la polisi, Ahamed Msangi amewataka wakazi wa jiji la Mbeya kuwa
watulivu akisema kuwa hakuna sababu za kufanya fujo kwa sababu
malalamiko ya madereva hao ni jambo linazozingumzika huku akidai kuwa
anaamini kikao cha dharura ambacho kimeitishwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya
Abaas Kandoro kikihusisha wadau wote wa usafirishaji kitatoa ufumbuzi wa
tatizo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni