STAND UNITED |
Kocha
Ally Jangalu wa Coastal Union amepelekwa kwenye kamati ya nidhamu baada
ya kuripotiwa kutoa matamshi ya kuidhalilisha TFF kwenye vyombo vya
habari kuwa Refa wa mechi kati yao na Ndanda SC iliyochezwa mjini Tanga
alikwenda na maelekezo ya kuhakikisha wapinzani wao wanashinda.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Kikao cha Kamati ya Kusimamia na Kuendesha ligi (Kamati ya Masaa 72), kufikia uamuzi huo.
Coastal Union ilifungwa bao 1-0 katika mechi hiyo iliyochezwa Februari 4, 2016. Suala lake linapelekwa Kamati ya Nidhamu.
Mchezaji
Daud Jumanne amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000
(laki tano) baada ya kumkanyaga vidole kwa makusudi mchezaji wa Simba
aliyekuwa akisubiri kupatiwa matibabu kwenye mechi kati ya timu hizo
iliyofanyika Februari 7, 2016 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga.
Adhabu
hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 37(3) ya Ligi Kuu Toleo la 2015.
Pia kwa kuzingatia Kanuni ya 37(20), hauruhusiwi kucheza mechi
inayofuata ya timu yake mpaka faini hiyo iwe imelipwa. Iwapo atacheza
kabla ya kulipa faini hiyo, timu yake itapoteza mchezo husika.
Klabu
ya Stand United imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kutoingia vyumbani
wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya African Sports iliyochezwa
Februari 6, 2016 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Kitendo hicho
ni kinyume na Kanuni ya 14(13) kuhusu taratibu za mchezo.
Kamishna
wa mechi hiyo namba 140, Idelfonce Magali amepewa karipio kwa
kutoripoti vizuri tukio hilo, wakati Refa Elly Sasii amepewa karipio
kali kwa kutoripoti kabisa tukio hilo.
CREDIT http://www.salehjembe.blogspot.com/
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni